HIYO picha ni ya wanandoa, Frank na Anita, hivi karibuni walifanya kumbukumbu ya miaka 81 ya ndoa yao.
Wazee hao walioana mwaka 1928
Kwa mujibu wa maelezo yao, yaani wanapendana utadhani wameanza uhusiano leo, kila mmoja anapenda kuwa na mwenzake popote anapokwenda na akimkosa hujiona kama kapungukiwa kitu fulani.
Kuna mdau kanitumia hii, isome inaweza kukusaidia
Umependeza!“Unajua siku hizi hunipendi” mwanamke ambaye ameishi na mume wake kwa miaka 6 alimlalamikia mume wake.
"Hivi unaongea kitu gani na wewe, kwa nini unasema hivyo hivyo?"
Mume naye alimjibu mke wake kwa kushangaa kwa nini mke wake anasema hampendi!
"Ni kweli hunipendi na siku zinavyozidi naona hunipendi zaidi" mwanamke aliendelea kulalamika.
Mshauri wa ndoa akaingilia kati na kumuuliza mume "je, huwa unamwambia mke wako Nakupenda?"
Kwa majivuno mwanaume akajibu kwamba
“Anajua nampenda, kila jioni nawahi nyumbani kuwa naye, nampa pesa anazohitaji anunulie kitu chochote anataka, nimemjengea nyumba nzuri, nimemununulia gari zuri, Pia nimekubali kuja naye kwako mshauri, je unadhani hadi hapo simpendi?
Mshauri akakaza uzi bado kwamba acha hayo yote je, huwa unamwambia “Nakupenda" mke wako?”
Mume akawa anamwangalia mke wake na mke akawa anatikisa kichwa kukubaliana na maneno ya mshauri wao wa ndoa kuonesha ni kweli huwa haambiwi na mume wake “nakupenda mke wangu.
Mume akajibu akasema “hivi kuna ulazima gani kumwambia nampenda wakati vitu ninavyofanya kwa ajili yake vinaonesha nampenda?"
Hapa wanaume wengi tunaweza kuandamana kumtetea mwanaume mwenzetu kwamba huyu mwanamke ana lake na kweli hana shukuruni.
Wanawake wangapi wamefanyiwa vile yeye amefanyiwa na wapo kimya, huyu
mwanamke pamoja na mazagazaga yote mwanaume mwenzetu amejitahidi kumpa bado anaonekana hampendi.
mwanamke pamoja na mazagazaga yote mwanaume mwenzetu amejitahidi kumpa bado anaonekana hampendi.
Hata hivyo linapokuja suala kuonesha mwanamke anapendwa tunatofautiana sana na mitazamo
Mwanamke huhitaji kusikia kwa maneno (tamka) over and over mkiwa wawili au hata mbele za watu kwamba unampenda au “nakupenda”.
Pia inaonekana ni jambo la kawaida sana, mwanzo wa kupendana watu huambiana maneno mengi matamu lakini wanavyoendelea na mahusiano huanza kujisahau.
Kuna maneno zaidi ya 16 ambayo wanandoa ni muhimu sana kuyatamka kila mmoja kwa mwenzake ili kuleta affections na msisimko wa kujisikia unapendwa hasa wanawake.
Itaendelea kesho.
No comments:
Post a Comment