MBUNGE wa Same Mashariki, Anne Kilango amesema, kuna udini na ukabila katika Bunge la Tanzania.
Kilango amesema kuwa, wabunge wameanza kuonyesha wazi kuwa wanataka kuwachagua viongozi kwa kuzingatia dini na makabila yao.
Mumewe,Mbunge wa Mtera,John Malecela ametahadharisha kwamba,upo uwezekano wa kutokea machafuko nchini kwa kuwa kun watu wachache wanaohodhi mali nyingi.
Wameyasema hayo nyumbani kwao, Sea View, Dar es Salaam, wakati wanapokea msaada wa vifaa vya walemavu kutoka Shirika la Hope Project for Disable Tanzania(HOPD) kwa kushirikiana na Kanisa la Christian Mission Fellowship kwa ajili ya jimbo la Mtera.
Kilango amewasihi viongozi wa dini wawafahamishe wananchi wa kuwapa mifano ya namna udini na ukabila vinavyoweza kupoteza amani ya nchi.
Ametoa changamoyto kwa watuhumishi hao wa Mungu kuhakikisha hilo linafanikiwa kama wanavyopiga vita ufisadi.
Malecela, amesema, machafuko yanaweza kutokea Tanzania kwa kuwa, watanzania wengi ni masikini, wachache wana mali nyingi.
Waziri Mkuu huyo Mstaafu amesema, kama Tanzania inataka iendelee kuwa nchi ya amani,lazima kuwe na mgawanyo sawa wa mali.
No comments:
Post a Comment