MUDA mfupi uliopita Naibu Spika wa Bunge, Anne Makinda, amewapiga promo ya nguvu wasanii wawili, Mzee Yusuf na Asia Idarous.
Kundi la taarab, Jahazi Modern Taarab lipo Dodoma, leo usiku linatarajiwa kuwachengua wabunge a.k.a waheshimiwa.
Idarous naye yupo ' Idodomya' kuwaonyesha waheshimiwa uwezo wake wa kubuni mavazi ya kanga.
Mzee Yusuf na Idarous walikuwa miongoni kwa wageni waliofika katika ukumbi wa Bunge leo asubuhi, Makinda aliwatambulisha.
Kama haitoshi, wamepewa promo free, waheshimiwa wametangaziwa kumbi zitakazotumika ukiwamo Royal Hotel (Mzee Yusuf) na Kilimani(Idarous), kazi kwenu waheshimiwa na wakazi wa Dodoma.
Deo Mwanambilimbi naye yupo Dodoma, nimepata taarifa kwamba bendi yake, Kalunde,ita-perform kwenye onyesho hilo la mavazi lililopewa jina la Usiku wa Kanga Dodoma.
No comments:
Post a Comment