LEO ni siku ya familia duniani lakini kwa bahati mbaya kuna taarifa zinazoshangaza kuhusu mwanamke jijini Dar es Salaam anayepita katika makazi ya watu na kuwavua chupi watoto.
Inadaida kuwa, mwanamke huyo hupita kwenye makazi hayo na kukaa nje ya nyumba kuwavizia watoto wanaocheza, akipata mwanya anawaita na kuwapeleka vichochoroni na kuwavua chupi zao.
Jina la mwanamke huyo halijafahamika, haijulikani anaishi wapi, na pia haifahamiki akizichukua anazipeleka wapi chupi hizo.
Hadi sasa ameshachukua chupi za watoto kadhaa jijini humo, na inasemekana kuwa anapenda chupi chafu.
Hivi karibuni alimbeba mtoto kwa lengo hilo hilo, mtoto akalia ikabidi amshushe na kutimua mbio, lakini alifanikiwa kuwavua watoto wawili katika mtaa mmoja.
Wazazi kuweni macho, kama upo ofisini waeleze walio nyumbani wawalinde watoto.
Huyo ana wenda wazimu wa mizimu ya kichaa cha kawaida tu kibinadamu au ulovi.
ReplyDeleteDarEsSalaama heshi vituko.