Tuesday, May 12, 2009

Mbagala salama

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, William Lukuvi amesema bomu lililolipuka jana lilikuwa la kutupwa kwa mkono na haikuwa bahati mbaya.
Lukuvi amesema, askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ) walilipua bomu hilo ili lisilete madhara.
Kwa mujibu wa Lukuvi, bomu hilo lilikutwa katika ghala la kuhifadhia silaha kwenye kambi ya JWTZ, Mbagala wilayani Temeke, Dar es Salaam wakati askari wakifanya usafi.
Wakazi wa Mbagala jana jioni walikumbwa na taharuki baada ya bomu hilo kulipuka, walikumbuka yaliyowakuta yalipolipuka mabomu mwisho wa mwezi uliopita na kusababisha madhara makubwa kwa kwao vikiwamo vifo.
RC Lukuvi kasema Mbagala ni salama, hakuna mabomu mengine yatakayolipuka hivyo wananchi wasiwe na wasiwasi.
Wakazi wa huko wanataka Serikali iwahamishe wakati inaendelea na mchakato wa kuwalipa fidia ili kujihadhari.

No comments:

Post a Comment