ASKARI wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ) wameanza kulipua mabomu katika kambi ya jeshi hilo Mbagala, Dar es Salaam.
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk Hussein Mwinyi jana aliwataka wananchi wakae mita zisizopungua 500 kutoka kambini hapo.
Dk Mwinyi amesema, JWTZ itateketeza mabomu 75 ya kutupwa kwa mkono, masalia ya risasi, baruti, viwashio na mabomu mengine ambayo hayakulipuka wakati ilipotokea milipuko ya mabomu kambini hapo.
Nimepata taarifa kwamba mabomu yanayolipuliwa sasa ni madogo, baadaye yatalipuka makubwa.
No comments:
Post a Comment