MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, William Lukuvi amesema, si kweli kwamba mabomu yaliyolipuka Mbagala yamesababisha watoto 200 wawe viziwi.
Lukuvi ameshangaa na kuhoji wlioandika taarifa hizo wamezipata wapi kwa kuwa, hakuna uchunguzi wowote wa kidaktari uliofanywa kuhusu tatizo hilo.
Amesema, taarifa hizo ni za 'uongo sana' na kwamba, mabomu yamewaathiri zaidi watu wazima na si watoto.
Kwa mujibu wa Lukuvi, waliokwenda hospitali kupata tiba ya athari za mabomu wengi ni watu wazima na kwamba watoto wapo OK.
Mabomu manne yalilipuka jana jioni, moja lililupka juzi jioni, na mengine mengi yalilipuka kwa bahati mbaya aprili 29 mwaka huu.
No comments:
Post a Comment