WATU wawili wamekufa leo saa mbili asubuhi Kibaha mkoani Pwani baada ya lori aina ya Scania kuligonga na kulipanda kwa juu basi dogo la abiria aina ya Toyota Hiece lililokuwa limesimama kupakia abira eneo la kwa Mathias.
Lori hilo lililokuwa limebeba kokoto, liligonga Hiece hiyo saa 2.40 asubuhi baada ya dereva wake, Juma Said Sufiani kushindwa kulimudu lilipopanda tuta lililopo barabarani.
Hiece hiyo yenye namba za usajili T 527 AVW ilikuwa katika kituo cha mabasi ikipakia abiria.
Baada ya kugongwa kwa nyuma iliburutwa takribani mita 10 pembeni ya barabara hadi mtaroni, ikapinduka, na lori kuipanda kwa juu.
Kamanda wa polisi mkoa wa Pwani, Absalum Mwakyoma amesema, watu wawili walikufa paop hapo, saba wamejeruhiwa, wanne kati ya hao hali zao ni mbaya wamekimbizwa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar es Salaam, dereva wa Hiece kavunjika mikono yote miwili.
Waliokufa ni mwanafunzi wa shule ya sekondari, na fundi umeme anayeishi Kibaha kwa Mathias.
Dereva wa lori amekamatwa yupo polisi, anatuhumiwa kuwa ni mzembe.
No comments:
Post a Comment