Thursday, April 2, 2009

Waliomuua Lucky Dube jela maisha


MAHAKAMA kuu nchini Afrika Kusini leo imewahukumu kifungo cha maisha raia watatu wa nchi hiyo baada ya kuthibitika kuwa walimuua kwa kumpiga risasi mwanamuziki nyota wa mahadhi ya raggae, Lucky Dube Oktoba mwaka 2007

Jaji wa Mahakama Kuu ya Gauteng jijini Johannesburg, Seun Moshidi, amewahukumu Sifiso Mhlanga(34) Julius Ngxowa( 32) na Mbuti Mabe( 31) ikiwa ni hukumu ya juu kabisa nchini humo.

Walipatikana na hatia katika mashitaka ya kujaribu kupora, na uhalifu mwingine.

Lucky Dube alikufa kwa kupigwa risasi akiwa na mwanae na imethibitika mahakamani kuwa Mhlanga ndiye aliyefyatua risasi zilizomuua.

Lucky Dube alikuwa mwanamuziki nyota wa raggae Afrika, hadi alipoaga dunia alikuwa amerekodi zaidi ya santuri 20.

No comments:

Post a Comment