Thursday, April 2, 2009

Nukuu za leo, haya nayo maneno!


"Mimi dhamira yangu ipo safi na tatizo hapa wabunge hawataki kuguswa mishahara wala posho zao" Dk Wilbroad Slaa.

"Bahati mbaya wabunge walipitisha lakini hawakuelewa wanapitisha nini, na hili ndiyo tatizo kubwa la wabunge wetu. Mara nyingi hupitisha mambo bungeni bila kujua wanapitisha nini" Dk Slaa.

"Namtafuta kwa simu Dk Slaa lakini hapatikani, nataka kumuuliza kama karukwa na akili..." Beatrice Shellukindo.

"Sisi wapinzani tulisema tukatwe asilimia 20 katika mapato yetu ziende kwenye mapato ya Serikali. Ningemwelewa Dk Slaa iwapo angelilia mapato haya lakini namshangaa kampeni hizi za kijinga anazofanya sasa"Hamad Rashid

"Kama ni makosa yalifanywa na nchi, mbona kuna samaki hawavuliwi, kuna dhahabu lakini wanapewa watu wachache? huwezi ku compare na mshahara wa Rais, mbona Rais anapokwenda nje ya nchi tu anapewa posho ya dola 500,000, mbona hawahoji?" Hamad Rashid.

No comments:

Post a Comment