Tuesday, April 7, 2009

"Nikifa mnizike na Jade"



Jade wakati anaumwa

MUME wa mtangazaji nyota wa vipindi halisi vya televisheni, Jade Goody(27), Jack Tweed(21) amesema akiaga dunia azikwe pembeni ya kaburi la mkewe ili wawe pamoja milele.

Jack aliyasema hayo akiwa pembeni ya kaburi la mkewe aliyefariki dunia kutokana na saratani ya mfuko wa kizazi.

Jack alikwenda eneo hilo jana, akakaa pembeni ya kaburi la Jade kwa dakika 30 huku akisali.

Kuna taarifa kwamba familia ya Jade imenunua eneo pembeni ya kaburi hilo hivyo siku moa huenda ndoto ya Jack itakuwa kweli.

No comments:

Post a Comment