Saturday, April 18, 2009

Mwandishi wa habari jela miaka 8



MAHAKAMA nchini Iran imemhukumu mwandishi wa habari kifungo cha miaka minane jela baada ya kupatikana na hatia ya kufanya ujasusi.

Msichana huyo, Roxana Saberi( 31) ana uraia wa nchi hiyo na Marekani, alikamatwa Januari mwaka huu kwa tuhuma za kutokuwa na vitambulisho vya kumruhusu kufanya kazi za uandishi wa habari nchini Iran.

Mapema mwezi huu mashitaka yalibadilishwa, akashitakiwa kwa kosa la kufanya ujasusi.

Mwandishi huyo ameishi Iran kwa miaka sita, amewahi kufanya kazi za kuviwakilisha vyombo mbalimbali vya habari nchini humo likiwamo Shirika la Utangazaji la Uingereza,BBC.

Wakili wake, Abdolsamad Khorramshahi amesema atakata rufaa. Utawala wa Obama umekuwa ukishinikiza aachiwe huru kwa kwa madai kuwa mashitaka hayo hayana msingi.

No comments:

Post a Comment