Thursday, March 5, 2009

Mwandishi wa habari afariki dunia


MWANDISHI wa habari wa kampuni ya Mwananchi Communications, Michael Uledi amefariki dunia usiku wa kumkia leo katika hospitali ya Mirembe, Dodoma.

Mwandishi mwenzake katika kampuni hiyo ofisi ya Dodoma, Faraja Jube amenieleza kuwa, taratibu kwa ajili ya mazishi na maziko zinaendelea, na kwamba atazikwa huko huko Dodoma.

Kwa mujibu wa Jube, Uledi ameacha mke na mtoto mmoja.

Uledi alizaliwa Mei 22, 1969, Buigiri, Dodoma, Mungu ailaze roho yake mahala pema peponi, amen.

No comments:

Post a Comment