Thursday, March 12, 2009

Aliyemzaba kibao Mwinyi adaiwa kudata






KIJANA anayedaiwa kumzaba kibao Rais Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Pili, Ally Hassan Mwinyi anadaiwa kuwa amedata baada ya kushindwa kwenda Ulaya.


Kwa mujibu wa gazeti la Serikali la Daily News la leo, kijana huyo alipohitimu kidato cha sita katika shule ya wavulana Tabora mwaka 2007 alitaka kuzamia Ulaya akashindwa.


Tangu wakati huo, kijana huyo mkazi wa Mabibo Farasi, Dar es Salaam, Ibrahim Said (26) anadaiwa kuwa na tabia zisizo za kawaida na kwamba, aliharibika’ alipokwenda kusoma Tabora.

Mjumbe wa nyumba 10 katika eneo analoishi kijana huyo amekaririwa akisema kuwa, siku moja aliwaeleza watu wakamuone mchumba wake nyumbani kwao, walipokwenda huko wakamkuta bibi yake!


Baada ya tukio hilo majirani walianza kuwa na mashaka na akili ya Said.

No comments:

Post a Comment