Tuesday, November 27, 2012

Sharo Milionea kuzikwa Tanga




Gari alilokuwa akiendesha Sharo Milionea
 
Muigizaji ambaye pia ni msanii wa muziki wa kizazi kipya, Hussein Ramadhani Mkiety maarufu kwa jina la Sharo Milionea, amekufa.

Kijana huyo maarufu, aliaga dunia jana  baada ya gari alilokuwa akiendesha kupinduka, akafa papo hapo. 


Alipata ajali jana jioni katika kijiji cha Lusanga, Muheza akiwa katika gari lenye namba za usajili T478 BVR Toyota Harrier. 

Kwa mujibu wa Polisi, wakati wa ajali, msanii huyo alikuwa pele yake kwenye gari.

Mwili wa marehemu Sharo Milionea upo katika Hospitali Teule ya Muheza.

Kijana huyo maarufu, aliaga dunia baada ya gari alilokuwa akiendesha kupinduka.

"Majira ya saa mbili usiku kwenye barabara ya Segera Muheza mtu mmoja alietambulika kwa jina la Hussein Ramadhani au Sharo Milionea akiwa anaendesha gari namba T478 BVR Toyota Harrier akitokea Dar es salaam kwenda Muheza alipofika eneo la Maguzonizonga wilayani Muheza hilo gari lake liliacha njia na kupinduka mara kadhaa na kusababisha kifo chake, mwili wa marehemu umehifadhiwa kwenye hospitali Teule ya wilaya ya MuhezaKamanda wa Polisi mkoa wa Tanga


Marehemu Sharo alianza kujipatia umaarufu baada ya kushiriki kwenye filamu za vichekesho zilizokuwa zikitayarishwa na msanii mkongwe wa fani hiyo, Amri Athumani maarufu kwa jina la King Majuto.

Baadaye alijitosa kwenye fani ya muziki wa kizazi kipya, ambapo alifanikiwa kuteka
soko la muziki huo baada ya kuibuka na kibao cha Chuki za nini.

 
Hivi karibuni, Sharo alijiongezea umaarufu zaidi baada ya kushiriki kutengeneza matangazo ya Kampuni ya Simu ya Airtel akiwa na King Majuto.

No comments:

Post a Comment