The scene where the Police Helicopter crashed in Ngong forest.
WAKENYA wameanza siku tatu za maombolezo baada ya kifo cha Waziri wa Usalama wa Kenya, Profesa George Saitoti, na naibu wake, Orwa Ojode.
Viongozi hao walikufa jana asubuhi kwenye ajali ya helikopta ya polisi katika eneo
la Ngong, nje ya Nairobi.
Rais wa Kenya, Mwai Kibaki amesema, kifo cha Bwana
Saitoti ni msiba mkubwa kwa taifa, na serikali imetangaza kuwa baraza la
mawaziri linakutana leo Jumatatu, kujadili tukio hilo.
"Ndege hiyo ya aina ya Eurocopter ya police
airwing, ambayo ilikuwa inaelekea Yugis, ilikuwa imembeba Waziri George
Saitoti, naibu waziri Orwa Ojode na maafisa rubani wa ndege, Nancy
Gitwanja na Luke Oyugi, na vilevile askari wawili ambao wanakuwa
wanaandamana na Waziri Saitoti, Inspector Tonkei na Thomas Murimi"
Saitoti aliwahi kuwa Makamu wa Rais na Waziri wa fedha katika serikali ya Rais Moi,.
Miili ya marehemu wote imeteketezwa kabisa na haitambuliki na hadi sasa chanzo cha ajali hiyo hakijafahamika.
Mawaziri hao wawili walikuwa wakielekea jimbo ambalo Orwa Ojode analiwakilisha bungeni la Ndhiwa, katika shughuli ya Harambee kulichangia kanisa moja huko.
Saitoti alikuwa miongoni mwa wanasiasa mashuhuri nchini Kenya waliokuwa wakipania kugombea kiti cha urais katika uchaguzi mkuu ujao.
Walioshuhudia ajali hiyo wamesema waliona helikota hiyo ikizunguka angani kabla ya kuanguka katika msitu wa Ngong.
No comments:
Post a Comment