Friday, June 22, 2012

Dk. Bilal aongoza Watanzania Mkutano wa Rio +20


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia katika Mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mazingira Endelevu (Rio+20) Juni 21, 2012  jijini Rio de Janeiro, nchini Brazil.

Mkutano huo ni wa pili kufanyika nchini humo tangu ulipofanyika kwa mara ya kwanza mwaka 1992.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Dkt. Terezya Huvisa, Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa rais wa Zanzibar, Fatma Fereji, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mahadhi Juma Maalim, wakiwa katika mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mazingira Endelevu (Rio+20) Juni 21,2012  jijini Rio de Janeiro, nchini Brazil.

Mkutano huo ni wa pili kufanyika nchini hapa tangu ulipofanyika kwa mara ya kwanza mwaka 1992. Picha na Muhidin Sufiani-OMR



Balozi Liberata Mulamula (kulia), akifurahia jambo baada ya kukutana na Mbunge wa Kahama ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya ardhi, Maliasili na Mazingira, James Lembeli, (wa pili kushoto), Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Sazi Salula (katikati), Mkurugenzi wa Mazingira, Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Julius Ningu, katika Viwanja vya Kumbi za mikutano ya Rio+20.
Picha na Muhidin Sufiani-OMR


No comments:

Post a Comment