Baadhi ya washiriki wa Semina ya
Wakuu wa Mikoa na Wilaya pamoja na Makatibu Tawala wa Mikoa
wakimsikiliza Waziri Mkuu, Mizengo Pinda wakati alipofungua kikao chao
kwenye Kituo cha Mikutano cha St. Gaspar Mjini Dodoma.(Picha zote na Ofisi ya Waziri Mkuu).
WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda amewataka wakuu wa mikoa na wilaya nchini kujiheshimu na kuacha kujiona
miungu watu.
Pinda pia amewataka viongozi hao wa Serikali kutokuwa walevi na wahuni.
,
Amewataka wawe kimbilio la wanyonge kwa kutenga nafasi za
kusikiliza kero za wananchi katika mikoa na wilaya wanazoongoza.
Aliwataka kuacha kufikiria kujinufaisha wao kwanza na kuwasihi
wakiona malalamiko na kero za wananchi zinafikishwa kwa Rais, Makamu wa
Rais na Waziri Mkuu, ni dhahiri kuwa viongozi hao hawatimizi wajibu wao.
"Haipendezi kwenda kwenye baa ya wazi, kabia kakikukolea unatoka
pale ukitaka usindikizwe… watu pale wamekuona sijui uko na mke au mume
wa mtu; mnatakiwa kuwa na mipaka, kunywa kabia kako jiheshimu, hata kama
unataka kudondoka basi dondoka kwa heshima," alisema.
"Mnatazamiwa kuonesha njia, nini kifanyike ili kukabiliana na
changamoto na malalamiko ya wananchi, mnatakiwa kuyapatia ufumbuzi
matatizo yanayowakabili badala ya kuwa sehemu ya matatizo hayo na ili
kufanikisha, kila mmoja atambue na akubali kuwa uongozi ni kufanya kazi
zaidi," alisema.
|
No comments:
Post a Comment