Monday, August 17, 2009

Tumia blog ya maisha unufaike

MAISHA ni blog isiyobagua, tangu ilipoanzishwa Februari mwaka huu imekuwa ikithamini kiu yako ya kupata taarifa kutoka pande zote za dunia.

Ukifungua blog hii utapata taarifa kuhusu masuala tofauti zikiwemo habari zenye mvuto za Tanzania zikiwemo taarifa kuhusu watu maarufu nchini, Afrika na maeneo mengine.

Ni blog yako kwa kuwa inagusa makundi yote kwenye jamii na inazingatia maadili ya taaluma ya uandishi wa habari.

Inasimulia habari kistaarabu na hutajilaumu kutumia sehemu ya muda wako kufungua www.simulizi.blogspot.com

Kila siku mamia ya watu ndani na nje ya Tanzania wanapata habari, wanaburudika na kuelimika kupitia blog ya MAISHA.
Itumie blog hii kufikisha taarifa yoyote unayoamini kwamba jamii inastahili kuifahamu.
Nitumie picha za matukio mbalimbali kama vile harusi, kipaimara, ubatizo, Sendoff, mahafali nk ili watu wengi ndani na nje ya Tanzania wazione kupitia blog hii.

Unaweza pia kuwakumbusha wenzako maisha yako ya siku zilizopita kwa kutuma picha zako ulizopiga shuleni, nyumbani, ofisini, na hata ulipokuwa mdogo.

Tafadhali tuma na maelezo yanayozihusu picha hizo ili iwe rahisi kuwafahamu wanaoonekana hapo ni akina nani, walikuwa wapi, wanafanya nini na lini.

Unaweza kupata rafiki kupitia blog hii, sema wewe ni nani, upo wapi, taja umri wako, jinsia yako, shughuli unayofanya, sema hobbies zako, elimu yako(si lazima) eleza unahitaji rafiki wa aina gani, awe na umri gani na ueleze pia mnaweza kuwasiliana vipi, mfano kwa njia ya simu, barua au barua pepe.

Unaweza pia kuitumia blog ya MAISHA kumpata mtu ambaye hamjaonana kwa muda mrefu. Kwa mfano mtu mliyesoma pamoja shule ya msingi, sekondari au chuoni, mtu ambaye mliwahi kuishi pamoja miaka ya nyuma lakini hamjaonana kwa muda mrefu, au mtu ambaye mliwahi kufanya kazi pamoja sehemu fulani lakini kwa muda mrefu hamjawasiliana au kukutana.

Si hivyo tu ,kama unahitaji wateja wa bidhaa yote, na endapo pia unahitaji bidhaa yoyote itumie blog hii ili utimize lengo lako.

Wakati wowote wasiliana nami kwa anuani ya barua pepe bmsongo@hotmail.com, www.simulizi.blogspot.com,au kwa namba za simu 0713-761 006, +255 22 2110595, 2127491/3

No comments:

Post a Comment