Monday, March 23, 2009

Unapokufa na mahari ya binti yako

MKAZI wa kitongoji cha Makazi Mapya mjini Sumbawanga amekufa mtoni wakati akitoka kuchukua mahari ya binti yake katika kijiji cha jirani.

Mzee Romano Michese(70) alitumbukia katika mto Kisa Machi 19 mwaka huu, akasombwa kwa umbali wa kilomita mbili na kukutwa amekufa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, Isunto Mantage amesema, alikuwa anatoka kuchukua mahari katika kijiji cha Mtimbwa, na alikunywa pombe kabla ya kuanza safari ya kurudi nyumbani, Makazi Mapya.

No comments:

Post a Comment