Thursday, February 26, 2009

Katibu Mkuu UN kawasili Tanzania

KATIBU Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Ban Ki-moon amewasili Dar es Salaam leo mchana kuanza ziara ya siku mbili bara na Zanzibar.

Ndege iliyomleta kiongozi huyo wa UN, wasaidizi wake, mkewe, Yoo Soon-taek, na waandishi wa habari ilitua katika uwanja wa ndege wa Julius Nyerere saa 8:54 mchana.

Waziri waMambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe aliwaongoza viongozi wa Serikali kumpokea Ban, Mratibu Mkazi wa Mashirika 17 ya UN yaliyopo nchini, Oscar Fernandez Taranco aliongoza ujumbe wa wafanyakazi wa mashirika hayo katika mapokezi hayo.

Viongozi kadhaa wa Serikali walishiriki kumpokea kiongozi huyo aliyetoka Afrika Kusini, wakiwamo Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira, Dk Batilda Burian, Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania UN, Balozi Augustine Mahiga, na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Patrick Tsere.

Baada ya kuteremka kwenye ndege ya UN, Ban na mkewe walipokea mashada ya maua, ukapigwa wimbo wa UN na wimbo wa Taifa la Tanzania, na alikagua gwaride.

Ban kesho anatarajiwa kwenda Zanzibar, atakuwa na mazungumzo na Rais Amani Abeid Karume, anatarajiwa kufungua ofisi za UN visiwani humo, atakwenda Arusha kutembelea Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari(ICTR), jioni yeye na mwenyeji wake, Rais Kikwete watazungumza na waandishi wa habari, leo usiku kiongozi huyo wa UN anatarajiwa kuondoka nchini.

1 comment:

  1. Hi! I could have sworn I've visited this web site before but after looking at
    some of tthe posts I realized it's new to me.Regardless, I'm definitely happy I discovered it and
    I'll be bookmarking it and checking back frequently!


    Feel free to visit mmy homepage ... rea

    ReplyDelete