NYOTA Waziri ni miongoni wa wanamuziki wanawake Tanzania wenye sifa ya pekee.
Ni mke wa kiongozi wa bendi ya The Kilimanjaro, maarufu kama wana Njenje, ni mwimbaji pekee mwanamke katika bendi hiyo iliyonzishwa miaka ya 1970's.
Kwa muda mrefu Nyota na mumewe, Waziri Ally wamekuwa wakitafuta mtoto, hadi sasa hawajafanikiwa, hawajakata tamaa.
Nimewahi kufanya mahojiano na Nyota nyumbani kwake Kijitonyama, Dar es Salaam, alibubujikwa machozi kwa sababu ya uchungu wa kukosa mtoto, inamuumiza.
Wapenzi wa Njenje wanamfahamu, sauti yake si mchezo, akiimba Gere ndo balaa, na siku hizi kabuni kitu, wakati wimbo huo unaisha wanawake hupata nafasi kuonyesha wanavyoweza kutumia nyonga zao.
Hutaja mikoa wanapotoka ili kuwaonyrsha wa mikoa mingine kuwa wao wapo juu, Nyota huwa huwahamasisha kwa kusema mfano, Tanga tupo juu, tupo juu, tupo juu, tup juu shitua waa!
Yote mipango ya Mola mtoa riziki, asisikitike sana, amshukuru tu Mungu kwa yote.
ReplyDelete