Bi. Arafa Issa Namaji
(Pichani) mwenye umri wa miaka 39 mkazi wa kijiji cha Narung’ombe
wilayani Ruangwa Mkoani Lindi anaomba msaada wa haraka utakaomuwezesha
kupata matibabu ya uvimbe ulio katika paji la uso.
Tatizo lilianza tangu February 2012, alianza kwa kuumwa na kichwa kwa maumivu makali sana na kipele kidogo kikatokea kwenye paji la uso, hivyo kadri kilipopungua maumivu ndipo kipele kiliendelea kuwa kikubwa hadi kuathiri macho na sehemu ya pua.
Baada ya kuona hali inazidi kuwa mbaya majirani na marafiki walimshauri kwenda hospitali ya wilaya, alipofika daktari alimpa rufaa ya kwenda hospitali ya Ndanda, hata hivyo Ndanda pia wakampa rufaa kwenda Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar es Salaam.
Kutokana na kuwa katika hali duni na hana mtu yeyote wa kumsaidia Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa wameichangishana kupata nauli pamoja na hela kidogo ya kujikimu kwa siku mbili, lakini bado anahitaji msaada zaidi wa pesa kwa sababu atahitaji kuishi zaidi Dar es Salaam, wakati akiwa katika hospital ya Muhimbili kwa ajili ya uchunguzi pamoja na matibabu yake.
Kwa aliye tayari kumsaidia anaweza kuwasiliana na Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoa wa Lindi ambae pia ni mwakilishi wa Channel Ten, Abdulaziz Ahmeid kwa namba za simu 0787176221 au 0756696048
No comments:
Post a Comment