Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne
Makinda (kushoto) na Naibu Spika Mhe. Job Ndugai (Mb) kwa pamoja wakiwa
na mazungumzo ya kina leo na ujumbe wa Tume ya Huduma za Bunge la Malawi
ulioko nchini hivi sasa, ambapo pamoja na mambo mengine walizungumzia
uhusiano mzuri wa mabunge ya nchi mbili hizi.
Kushoto kwa Mhe. Ndugai ni
Naibu Spika wa Bunge la Malawi Mhe.Juliana Mpande (Mb) ambaye ni mkuu
wa msafara. Wengine ni Kamishna Alfred Mwechumu (Mb) na Kamishna
Christina Chiwowo (Mb).
Spika wa Bunge la Tanzania akiwa na
mazungumzo na Uongozi wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam waliofika ofisini kwake Dodoma leo. Spika Makinda amewataka na
kuwaasa kuwa na uzalendo kwa nchi yao.
Picha na Prosper Minja - Bunge
No comments:
Post a Comment