Monday, August 27, 2012

Makamu wa Rais ashiriki sensa

 Makamu wa Rais,Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Ofisa kutoka Ofisi ya Takwimu ya Taifa, Radegunda Maro, wakati ofisa huyo alipofika nyumbani kwa kiongozi huyo akiwa na Karani wa Sensa na msimamizi wake kutoka Kituo cha Oysterbay, Dar es Salaam kwa ajili ya kukamilisha Sensa, jana asubuhi.
 Makamu wa Rais, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akijiandaa kujibu maswali kutoka kwa Karani wa Sensa, Happyness Masaka yanayohusu sensa ya watu na makazi.
Makamu wa Rais, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Karani wa Senza, Happyness Masaka, baada ya kujibu maswali yanayoihusu familia yakejana asubuhi nyumbani kwake Oysterbay, jijini Dar es Salaam. 
 
Kulia ni Msimamizi wa Sensa wa Kituo cha Oysterbay, Daria Kailembo (kushoto) ni Ofisa kutoka Ofisi ya Takwimu ya Ttifa, Stanley Mahembe

No comments:

Post a Comment