Friday, August 10, 2012

Balozi Costa Mahalu baada ya kuachiwa huru Kisutu


 Aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Italia, Prof. Costa Mahalu akikumbatiana na mdogo wake Vilasi Rama baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, kumuachia huru katika kesi ya kuhujumu uchumi iliyokuwa ikimkabili.
 Prof.Costa Mahalu katikati akitoka nje ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es salaam huku akiongozana na wakili wake, Mabere Marando (kushoto).
  Prof.Costa Mahalu akipeana mkono na ndugu na jamaa waliofika mahakamani.
 Prof.Costa Mahalu akizungumza na waandishi wa habari nje ya Mahakama ya Kisutu, Dar es Salaam.
 Aliyekuwa Ofisa utawala katika ubalozi wa Tanzania nchini Italia, Grace Martin akitoka Mahakamani. 
Kwa hisani ya blog ya Francis Dande

No comments:

Post a Comment