Mkurugenzi
wa Tanzania One Thetre (TOT) ambaye pia ni Mbunge wa Mbinga Magharibi,
John Komba akizungumzia hali ya afya yake, alipowaita waandishi wa
habari, nyumbani kwake, Mbezi Tangi Bovu, Kawe, Dar es Salaam, leo,
Julai 27, 2012. Kushoto ni Mkewe, Salome Andrew Komba.
Sehemu aliyofanyia upasuaji wa nyonga
MKURUGENZI
wa Kundi la Tanzania One Theatre (TOT) ambaye pia ni Mbunge wa Mbinga
Magharibi, John Komba amerejea kutoka India ambako amefanyiwa upasuaji
kumtibu ugonjwa wa nyonga ulilokuwa ukimsumbua upande wa mguu wake wa
kulia.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo Julai 27, 2012, nyumbani kwake Mbezi kwa
Komba, mjini Dar es Salaam, Komba alisema amerejea nchini, Juzi, baada
ya kupatiwa matibabu hayo kwenye hospitali ya Appolo iliyopo Hydrabad
nchini India tangu mwanzoni mwa wezi huu.
Alisema,
aliondoka nchini, Julai 2, 2012, baada ya kupelekwa na serikali kwa
maelekezo ya Rais Jakaya Kikwete, Spika wa Bunge Anna Makinda na Katibu
wa Bunge John Kashilila na kwamba alikwenda baada ya kukosa matibabu
hapa nchini kwa sababu ya mgomo wa madaktari.
"Siku
napelekwa Muhimbili tu, tayari madaktari walikuwa wameanza siku ya
kwanza ya mgomo wao, nikawa sina namna ila kuujulisha uongozi wa Bunge
na kisha nikamuomba Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, naye kwa
mamlaka yake akanisaidia haraka kama ambavyo huwasaidia wengine kwenda
kutibiwa nje", alisema Komba.
Alisema,
uzito ulichangia sana kusababisha mifupa kusagana kwenye nyonga upande
wa mguu wa kulia, ambapo hadi anakwenda India alikuwa na uzindo wa kilo
138 wakati wastani wa uzito aliotakuwa kuwa nao kulingana na ukumbwa wa
mwili wake ni kilo 90 au 100 tu.
Picha kwa hisani ya Mseto Blog.
No comments:
Post a Comment