Kikosi cha Stars jana |
MECHI
ya mchujo ya Kombe la Dunia Kanda ya Afrika kati ya Tanzania (Taifa
Stars) na Gambia (The Scorpions) iliyochezwa Juni 10 mwaka huu Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam imeingiza sh. 124,038,000.
Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniphace Wambura Mgoyo amesema leo kwamba, mapato hayo yametokana na washabiki 31,122 waliokata tiketi
kushuhudia pambano hilo kwa viingilio vya sh. 3,000, sh. 5,000, sh.
10,000, sh. 20,000 na sh. 30,000. Washabiki 25,901 walikata tiketi za
sh. 3,000.
Amesema
asilimia 18 ya mapato hayo ambayo ni sh.
18,921,050.85 ilikwenda kwenye
Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) wakati gharama kabla ya mgawo
zilikuwa tiketi (sh. 6,555,000), bonasi kwa Taifa Stars (sh.
15,767,542.37), waamuzi (sh. 13,372,000), usafi na ulinzi (sh.
2,350,000), maandalizi ya uwanja- pitch preparation (sh. 400,000),
Wachina- Beijing Construction (sh. 2,000,000), umeme (sh. 300,000) na
mafuta ya jenereta (sh. 200,000).
Amesema kwa
upande wa mgawo asilimia 20 ya gharama za mechi ni sh. 12,834,481,
asilimia 10 ya uwanja sh. 6,417,241, asilimia 5 ya Shirikisho la Mpira
wa Miguu Afrika (CAF) sh. 3,208,620, asilimia 20 ya Mfuko wa Maendeleo
ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 12,834,481 na asilimia 45 ya TFF (sh.
28,877,583).
Chanzo: blog ya bongostaz
No comments:
Post a Comment