Mbunge wa Maswa Mashariki, John Shibuda (Chadema) ametoa siku tatu na kulitaka Baraza la
Vijana Chadema (Bavicha) limwombe radhi kwa madai kuwa limemdhalilisha.
Shibuda amesema, Bavicha lisipofanya hivyo, atalishitaki
kwa wapiga kura wake ambao watatoa msimamo wao.
Kwa mujibu wa Mbunge huyo, kinachomponza ndani ya Chadema ni yeye kuwa Msukuma na amehoji amefanya dhambi gani kutangaza kuwa atagombea urais.
Amewaeleza waandishi wa habari mjini Dodoma kuwa, hatakubali kuwa ‘kitoweo’ cha wajinga ndio waliwao na amesisitiza kwamba, azma yake ya kugombea urais iko pale pale.
"Niko tayari kupoteza maisha yangu kwa kupigania utu wangu, uchaguzi
mkuu wa mwaka 2010 nilizunguka na Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Willibrod
Slaa katika Kanda ya Ziwa nikamnadi kuwa anafaa kuwa Rais, sasa
najiuliza kazi yangu ni kutangaza wengine wagombee urais?
“Kama chama kitanipitisha kugombea urais nitagombea na itakuwa zamu ya Dk. Slaa kunipigia debe," alisema Shibuda.
Alisema, amesikitishwa na kauli za Mwenyekiti wa Bavicha, John Heche, baada ya kutangaza kuwa atagombea urais 2015 kwa tiketi ya Chadema na kauli za kumbeza na kuonekana hafai zimekuwa zikitolewa dhidi yake bila kuulizwa.
"Heche lazima aniombe radhi kwa kunikashifu mbele ya Watanzania, lakini hapo ndipo desturi ya mtu mzima ovyo inapothibitika, kwani mtu unatakiwa kuchunguza kwanza kabla ya kusema," alisema Shibuda.
“Nawaomba wananchi wawe watulivu hasa wapiga kura wangu, kwani kama kuna mabaya yanatakiwa yatoke ulimini mwangu, na si mtu kunisemea; matakwa ya kauli ya Bavicha ni kifuniko cha siri sana na kama wanaona kutangaza kwangu kugombea urais ni vibaya ni bora watangaze nani wanamtaka agombee nafasi hiyo kupitia Chadema.
"Inasikitisha, Mwenyekiti wa Baraza anatangaza dhambi ya kubaguana, kuna dhambi gani Shibuda kusema kusudio lake la kugombea urais? Tabia aliyoonesha Mwenyekiti inatambulisha huzuni ya fikra mtambuka, kuwa hakuna mtu anayeweza kuchaguliwa bila kura mchanganyiko," alisema.
Alisema wameamua kumchokoza kupitia vyombo vya habari, kwani akiwa kwenye semina ya Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, iliyokuwa imeandaliwa na Mpango wa Kutathimini Utawala Bora Afrika (APRM) mwanzoni mwa wiki mjini Dodoma, Rais Jakaya Kikwete alimwuliza kama atagombea urais akamjibu.

Alisema yeye ni miongoni mwa watu walioingiza wanachama wengi Chadema na hata Dk. Slaa alipogombea urais 2010 hakupigiwa kura na wanachama wa Chadema peke yao, kwani wapo hata wana CCM waliompigia lakini anashangaa dhambi ya ubaguzi ilikotoka.
Alisema katika uchaguzi wa Bunge la Afrika Mashariki hivi karibuni, Chadema ilikuwa na mgombea Anthony Komu na alikwenda kuomba hata watu wa CCM wampigie kura, lakini hakusikia akionywa kwa nini alifanya vile.
"Leo Msukuma Shibuda, anatoa kauli ile ile inakuwa haramu, je Mtanzania ajifunze nini? Labda ningekuwa Mchaga nisingeulizwa, inasikitisha sana," alisema.
“Hata nikifukuzwa ndani ya chama hicho, watakaofanya hivyo watakuwa wamepata faida gani? Lakini hilo litathibitisha uongozi wa Chadema kuwa wa kidikteta na nawaomba viongozi wa Chadema watafakari kwa kina bila jazba, kwani tabia waliyoonesha vijana wa Chadema haipendezi hata kidogo.
"Juzi nilimpigia simu Mbowe (Freeman) na kumwuliza kama aliwatuma vijana wanitukane, akasema atanipigia lakini mpaka sasa hajafanya hivyo," alisema.
Shibuda alisema kama alikosea kujiunga Chadema atawataka radhi Watanzania.
"Mwaka 2005 nilipotangaza kugombea urais kupitia CCM hakuna aliyenishangaa Umoja wa Vijana au Wanawake hawakunichafua, si NEC ya CCM, au Kamati Kuu na wala sikutishwa kufukuzwa kwenye chama, sikupewa sifa za ajabu, iweje iwe hivyo Chadema ambacho ni Chama cha Demokrasia na Maendeleo?"
No comments:
Post a Comment