Monday, May 7, 2012

‘Nikimuona mtu ana kamera natamani kumtafuna’


Mzee mwenye umri wa miaka 90 mkazi wa Dodoma aliyetajwa kwa jina la John Mkweji ni adui wa kamera na hataki hata kuziona.

Mzee huyo mkazi wa Kata ya Iringa Mvumi pia hataki kusikia habari zozote kuhusu Mungu.

Inadaiwa kuwa mzee huyo anaamini kwamba, kamera ni sumu kwake, na kwamba akiona tu mwanga wa kifaa hicho atakufa.

Amemweleza mwandishi wa habari hizi kuwa, alijenga uadui na kamera wakati akiwa ni miaka 30’s yakiwa ni matokeo ya tiba aliyopewa na mganga wa kienyeji.

Mganga huyo alimpa John dawa mbili zilizotajwa kwa majina ya pusha na Pundugwa ili zimwezeshe kumlinda afanikishe mambo ya uhalifu anayodaiwa kuyafanya wakati huo.

Mzee huyo alimweleza mwandishi wa habari hizi kwamba, alikuwa na bahati kuzungumza naye wakati akiwa na kamera, kwa kuwa, anapomuona mtu akiwa na kifaa hicho huwa anatamani kumtafuna.

No comments:

Post a Comment