RAIS Jakaya Kikwete ametangaza baraza jipya la mawaziri na
kuwatupa nje mawaziri SITA akiwemo Mustafa Mkulo.
Rais Kikwete amesema, makatibu wakuu na wakurugenzi wote ambao wizara na
idara zao zilihusishwa na tuhuma za ufisadi watawajibishwa.
Mkulo alikuwa Waziri wa Fedha, Rais Kikwete pia amemtosa aliyekuwa
Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, na Waziri wa Maliasili na
Utalii, Ezekiel Maige.
Mawaziri wengine waliotemwa ni pamoja na Omari Nundu aliyekuwa Waziri
wa Uchukuzi, ambaye sasa nafasi yake inachukuliwa na Dk. Harrison
Mwakyembe.
Aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara,Dk. Cyril Chami naye kaachwa, amerithiwa na Abdallah Kigoda.
Nundu ameondoka na Naibu wake, Athuman Mfutakamba, ambaye
alimshambulia waziwazi kwa tuhuma za kuhusika kuibeba kampuni ya moja ya
Kichina.
Aliyekuwa Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Lazaro
Nyarandu, kabaki, sasa anakuwa Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii.
Wengine waliotemwa ni aliyekuwa Waziri wa Afya Dk. Haji Mponda na
Naibu wake, Lucy Nkya, ambao waliingiza nchi katika mgogoro mkubwa wa
mgomo wa madaktari.
Mawaziri wawili tu kati ya waliotuhumiwa na wabunge
kwa ufujaji wamenusurika katika mchujo huo.
Hao ni aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa
na Serikali za Mitaa, George Mkuchika, ambaye sasa anakuwa Waziri, Ofisi
ya Rais Utawala Bora, na mwingine ni aliyekuwa Waziri wa Kilimo na
Chakula, Prof. Jumanne Maghembe ambaye amehamishiwa Wizara ya Maji.
Katika uteuzi huo, Kikwete aliingiza sura mpya na zisizofahamika
katika duru za siasa, akiwemo mtu pekee ambaye atakuwa amevunja rekodi
ya kupanda vyeo kwa kasi, Saada Mkuya Salum, ambaye jana mchana
aliteuliwa kuwa mbunge, na saa chache baadaye kutangazwa kuwa Naibu
waziri wa Fedha.
Mawaziri wapya walioingizwa katika baraza jipya ni pamoja na Mbunge
mpya, Prof Sospeter Muhongo, ambaye sasa anakuwa Waziri wa Nishati na
Madini, na Waziri wa Fedha, Dk. William Mgimwa.
Mawaziri wengine na nafasi zao katika mabano ni
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu) Stephen M. Wasira, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utumishi) Celina Kombani, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano), Samia H. Suluhu na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Dk. Terezya P.L. Huvisa.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji na Uwezeshaji)
itaendelea kuwa chini ya Waziri Mary M. Nagu, wakati Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI) sasa itashikwa na Hawa Ghasia. Waziri
William Lukuvi anaendelea na nafasi yake ya Sera, Uratibu na Bunge.
Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, itaendelea kuongozwa na
Samuel J. Sitta, wakati Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa sasa
atakuwa Shamsi Vuai Nahodha.
Waziri wa Ujenzi ni yule yule John P. Magufuli, wakati Dk. Huseein A.H. Mwinyi amerudishwa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.
Mawaziri wanaoendelea na wizara zao ni pamoja na Waziri wa Elimu na
Mafunzo ya Ufundi Dk. Shukuru J. Kawambwa, Waziri wa Maendeleo ya Jamii,
Jinsia na Watoto, Sophia M. Simba, Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard K. Membe, Waziri wa Maendeleo ya
Mifugo na Uvuvi Dk. David M. David, Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudentia
M. Kabaka na Waziri wa Mawasiliano, Sayansi, Teknolojia Prof. Makame M.
Mbarawa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Prof. Anna
K. Tibaijuka,
Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika atakuwa, Christopher Chiza,
ambaye awali alikuwa naibu wa wizara hiyo.
Waliohamishwa wizara ni Waziri wa Katiba na Sheria, Mathias M.
Chikawe, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Emmanuel Nchimbi, Waziri wa
Maji Prof. Jumanne Maghembe, Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo Dk. Fenella E. Mukangara, Waziri wa Maliasili na Utalii, Khamis
Kagasheki, wakati Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe, na Prof
Mark Mwandosya anakuwa Waziri asiyekuwa na Wizara Maalum.
Sura mpya za manaibu mawaziri ni pamoja na George Simbachawene
anayekuwa Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Januari Makamba anayekuwa
Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Amos Makala
anayekuwa Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Naibu
Waziri wa Fedha, Saada Mkuya Salumna Naibu Waziri wa Fedha, Janet Mbene.
Manaibu wengine ni Naibu Waziri wa Uchukuzi, Charles J. Tizeba, Naibu
Waziri wa Maji, Dk. Binilith Mahenge, Naibu Waziri Nishati na Madini,
Stephen Maselle, na Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Angela Jasmine
Kairuki.
Wengine ni Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais, Charles Kitwanga,
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Elimu), Majaliwa K.
Majaliwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI), Aggrey
Mwanry.
Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Dk. Makongoro M. Mahanga, Naibu Waziri
wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Adam Malima, aliyeondolewa wizara ya
Madini na Nishati, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira A.
Silima, na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Gregory G. Teu.
Wengine ni Naibu Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Benedict N.
Ole-Nangoro, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,
Mahadhi J. Maalim, Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya
Makazi, Goodluck J. Ole-Medeye, Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii,
Jinsia na Watoto, Ummy A. Mwalimu, Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya
Ufundi, Philipo A. Mulugo, Naibu Waziri wa Ushirikiano wa Afrika
Mashariki, Dk. Abdulla Juma Abdulla, Naibu Waziri wa Ujenzi, Gerson
Lwenge na Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Suleiman
Rashid.
No comments:
Post a Comment