Friday, April 27, 2012

Tundu Lissu ashinda kesi ya ubunge

Mahakama Kuu Kanda ya Singida leo imemtangaza Tundu Lissu kuwa ni Mbunge halali wa Singida Mashariki (Chadema).

 

Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Kabwe Zitto (Chadema), amepongeza Lissu.

 

'Kamanda Tundu Lissu ameshinda kesi dhidi yake. Mahakama Kuu Singida imemtangaza rasmi ndg. Tundu Lissu kuwa mbunge halali wa jimbo la Singida Mashariki. Hongera kamanda' amesema Zitto kwenye ukurasa wake wa facebook.

 

Mbunge wa Ubongo, John Mnyika (Chadema), ameandika maneno yenye maana kwamba, nguvu ya Mungu ndiyo iliyomuwezesha Lissu ashinde kesi hiyo.

 

'Kama yu pamoja nasi, nani awezaye kutushinda?' amesema Mnyika kwenye ukurasa wake kwenye facebook.

No comments:

Post a Comment