Friday, April 27, 2012

Jokate achukua nafasi ya Wema kwa Diamond

 Jokate

Diamond na Wema

 

HATIMAYE imethibitika kwamba, mwanamuziki Naseeb Abdul Jumaa ‘Diamond Platinumz,’ ana uhusiano wa kimapenzi na Miss Tanzania namba 2, 2006/07, Jokate Mwegelo.

 

Diamond alitumia mtandao wa BBM kuthibitisha kuwa anampenda Jokate kupitilizaaa....

 

‘No wan can take your place Kate..I love you so much my baby..’, jambo lililoibua mshtuko kwa waliyoona maneno ya Diamond ambaye bila shaka ndiye msanii namba moja kwa sasa Bongo.

 

Kwa mara ya kwanza Diamond amekiri kwamba Jokate ni la aziz wake.

 

“Ni kweli niko in love (ndani ya penzi) na Kate (Jokate) ila bado sijapanga siku ya kumtambulisha rasmi kwa mashabiki wangu ili wamfahamu shemeji yao.”

 

“Nampenda sana Jokate, hakuna wa kuchukua nafasi yake.”

 

Mwishoni mwa mwaka jana, aliyekuwa mchumba wa Diamond, Wema Isaac Sepetu alitangaza vita na Jokate akimtuhumu kumwingilia kwenye penzi lake na Diamond.

 

Hivi karibuni Diamond alisema,kwa sasa ana mpenzi mpya ambae si maarufu kabisa.

 

“Tuna kama mwezi hivi toka tumeanza kuwa pamoja, sio vizuri sana kumzungumzia kwa sababu naogopa sana drama mwisho yasije yakawa yale yale tena ndio maana nafanya siri lakini sio maarufu na wala sio Jokate.”alisema Diamond.

 

Alipoulizwa kama ataingia tena kwenye mapenzi na mtu maarufu ambako ndiko alikotoka, Diamond amesema “kwa kweli siwezi kujua kwa sababu kila kitu kinaandikwa na mapenzi ni kama ajali.”

 

Diamond aliwahi kukanusha kwamba hana uhusiano wa kimapenzi na mrembo Jokate ambae walianza kuzungumziwa sana baada ya Jokate kushuka kwenye gari moja na Diamond wakati wakiwasili kwenye show ya Mlimani City wiki kadhaa zilizopita.

 

Kwenye hiyo benz alishuka Diamond na mama yake mzazi pamoja na Jokate na Diamond alipoulizwa alisema siku hiyo alitakiwa kushuka na mamodo wawili lakini mmoja ambae ni Lisa alishindwa kuja siku hiyo kwa hiyo ikabidi ashuke na Jokate tu.

 

Wakati Diamond akizindua album yake ya LALA SALAMA ndani ya maisha club, Dar es Salama aliruhusu watu kuuliza maswali kibao waliyokuwa na o na kuyajibu moja baada ya jingine. Diamond alifunguka na kusema kuwa yeye hana uhusiano na JOKATE na ni dada yake ila Wema ndio ubavu wake.

No comments:

Post a Comment