Mmoja wa wajumbe wa tume ya mabadiliko ya Katiba walioapishwa jana Ikulu, Dar es Salaam, alikataa kushika kitabu chochote cha dini, wakati akiapishwa.
Wengine ni Humphrey Polepole, Yahya Msulwa, Esther Mkwizu, Maria Kasonda, Al-Shaymaa Kwegyir na Mwantumu Malale pamoja na Joseph Butiku.
Profesa Mwesiga Baregu alikataa kushika Biblia au Kurani kama walivyofanya wajumbe wengine.
Wajumbe wengine walishika moja ya vitabu hivyo kulingana na imani yao lakini yeye alivikataa, na wakati anaapa aliweka mkono wake kifuani kwake na kutamka maneno ya kiapo katika karatasi maalumu iliyokuwa imeandikwa.
Uamuzi wa Baregu uliwashangaza wageni wengi, akiwemo Rais Kikwete mwenyewe ambaye alionekana akitabasamu.
Baregu anakuwa Mtanzania wa pili, baada ya Kingunge Ngombale Mwiru ambaye kwa miaka yote amekuwa akiapa mikono mitupu.
Wajumbe wengine walioapa kwa kushika vitabu vya Biblia au Kurani kulingana na imani yao, ni pamoja na Mwenyekiti wake Jaji mstaafu Joseph Warioba, Makamu Mwenyekiti Jaji mstaafu Augustino Ramadhani ambao walishika Biblia.
Wajumbe walioapishwa ni Riziki Shahari Mngwali, Dk. Sengodo Mvungi, Richard Lyimo , John Nkolo, Alhaj Said EL- Maamry, Jesca Mkuchu, na Profesa Palamagamba Kabudi.
Wengine ni Humphrey Polepole, Yahya Msulwa, Esther Mkwizu, Maria Kasonda, Al-Shaymaa Kwegyir na Mwantumu Malale pamoja na Joseph Butiku.
Aidha Kikwete aliwaapisha pia Dk. Salim Ahmed Salim, Fatma Said Ali, Omar Sheha Mussa, Raya Suleiman Hamad, Awadh Ali Saidi, Ussi Khamis Haji, Salma Maoulid, Nassor Khamis Mohammed, Simai Mohamed Saidi, Muhammed Yussuf Mshamba, Kibibi Mwinyi Hassan, Suleiman Omar Ali, Salama Kombo Ahmed, Abubakar Mohammed Ali, Ally Abdullah Ally Saleh.
Watendaji wa tume walioapishwa ni Katibu wake Assaa Ahmad Rashid na Naibu Katibu wake Casmir Sumba Kyuki.
Watendaji wa tume walioapishwa ni Katibu wake Assaa Ahmad Rashid na Naibu Katibu wake Casmir Sumba Kyuki.
No comments:
Post a Comment