WAZIRI wa Ujenzi, Dk. John Magufuli, jana aling’aka akidai kuwa mwenye majibu kuhusiana na tuhumu zilizoelekezwa kwake na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, juzi za kutumia vibaya madaraka yake na kutisha wananchi ni Waziri Mkuu Mizengo Pinda.
Dk. Magufuli alitoa majibu hayo alipotakiwa na Tanzania Daima kutoa maelezo juu ya tuhuma hizo alizotupiwa pamoja na mawaziri wenzake watatu.
Wakati mawaziri wenzake wakitoa maelezo yao nje ya ukumbi wa Bunge kwa nyakati tofauti, Dk. Magufuli alikuja mbogo baada ya kuulizwa na kisha kujibu kwa mkato kuwa akaulizwe Waziri Mkuu.
“Sina la kukujibu, suala hilo kamuulize Waziri Mkuu kwani ndiye aliyeulizwa jana,’’ alisema.
Mbowe alimtaka Pinda atoe tamko rasmi ikiwa ndilo agizo na maamuzi ya serikali na kujua yalitolewa lini na katika kikao gani.
Hata hivyo, hoja hiyo ilimchefua Pinda ambaye kwanza alikana kuwepo kwa kauli hizo na kisha kueleza kusikitishwa kwake na hatua ya Mbowe kutoa matamshi hayo akiwa kama mmoja wa viongozi wakuu wa kisiasa nchini.
Kiongozi mkuu akijitetea, Waziri Nagu alishindwa kukubali au kukataa na kuelezea kuwa alichozungumza kilikuwa ni siasa.
“Arumeru tulikuwa kwenye mapambano, hivyo kila mmoja anatumia silaha yake na wala sikutumia gari la uwaziri,” alisema Nagu ambaye ni mbunge wa Hanang.
Kwa upande wake, Medeye alidai hakumbuki kama aliwahi kutoa kauli hizo na kueleza kwamba kama Mbowe ana ushahidi aupeleke bungeni.

Juzi, Mbowe akiuliza swali la papo hapo kwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, aliwalipua mawaziri John Maghufuli, Dk. Mary Nagu, Stephen Wassira na Goodluck ole Medeye kwa madai kuwa wamekuwa wakitoa kauli za kibaguzi na vitisho kwa wananchi waliowachagua wagombea wa upinzani wakati wa kampeni.
Mbowe alimtaka Pinda atoe tamko rasmi ikiwa ndilo agizo na maamuzi ya serikali na kujua yalitolewa lini na katika kikao gani.
Hata hivyo, hoja hiyo ilimchefua Pinda ambaye kwanza alikana kuwepo kwa kauli hizo na kisha kueleza kusikitishwa kwake na hatua ya Mbowe kutoa matamshi hayo akiwa kama mmoja wa viongozi wakuu wa kisiasa nchini.
Kiongozi mkuu akijitetea, Waziri Nagu alishindwa kukubali au kukataa na kuelezea kuwa alichozungumza kilikuwa ni siasa.
“Arumeru tulikuwa kwenye mapambano, hivyo kila mmoja anatumia silaha yake na wala sikutumia gari la uwaziri,” alisema Nagu ambaye ni mbunge wa Hanang.
Nagu alisema alikwenda katika uchaguzi mdogo wa Jimbo la Arumeru Mashariki kukisaidia chama chake na hasa ikizingatiwa kuwa jimbo hilo liko jirani na lake.
Pamoja na majibu hayo, alimshauri Mbowe kuachana na maneno yanayotolewa wakati wa kampeni, kwani yanakuwa mengi na kwamba yakifuatwa yanaweza kusababisha kutoweka kwa amani nchini. Hakufafanua.
Kwa upande wake, Medeye alidai hakumbuki kama aliwahi kutoa kauli hizo na kueleza kwamba kama Mbowe ana ushahidi aupeleke bungeni.
“Sikumbuki kutoa kauli kama hiyo, lakini kama Mbowe ana ushahidi wa mikanda ya video alete bungeni ili ukweli ujulikane,’’ alisema.
Hata hivyo, alisema kuwa tangu alipoteuliwa kuwa Naibu Waziri amekuwa akifanya kazi bila upendeleo na hata kuyatembelea majimbo ambayo yanaongozwa na upinzani.
Juzi Mbowe alisema mawaziri hao na viongozi wengine wa CCM wamekuwa wakitoa kauli za kuwatisha wananchi kuwa wakichagua vyama vya upinzani maeneo yao hayatapatiwa fedha za maendeleo.
Alisema Nagu alitoa kauli hiyo Arumeru, Medeye aliitoa Arusha na Magufuli wakati wa kampeni Igunga.
Chanzo: Gazeti la Tanzania Daima
No comments:
Post a Comment