Friday, April 13, 2012

Msichana anywa sumu amfuate marehemu Kanumba

Mmoja wa waombolezaji waliopoteza fahamu wakati wa mazishi ya Kanumba
Jeneza lenye mwiili wa Steven Kanumba


Msichana mkazi wa Misugusugu wilayani Kibaha Mariam Elias (19) atashitakiwa mahakamani kujibu mashitaka ya kutaka kujiua kwa kukusudia.


Binti huyo amekiri kutaka kujiua kwa sababu ya uchungu aliopata kutokana na kifo cha msanii nyota wa filamu nchini Tanzania, Steven Kanumba.


Mariam amekiri kutaka kujiua kwa kunywa sumu ya panya kwa kile alichokielezea kuwa ni masikitikio yake kutokana na kifo cha Kanumba.


Kanumba aliaga dunia usiku wa kuamkia Aprili 7 nyumbani kwake, Sinza, Dar es Salaam.

Mariam yupo chini ya ulinzi katika hospitalini Tumbi, Kibaha anapoendelea na matibabu.

Binti huyo alikaririwa na vyombo vya habari jana kuwa aliomba Sh 200 kwa rafiki yake na kwenda kununua sumu ya panya na kuinywa kutokana na majonzi makubwa aliyonayo kwa kifo cha Kanumba.


Kwa mujibu wa msichana huyo, kifo hicho cha Kanumba kimemuumiza kiasi cha kuona bora anywe sumu ili aondoke duniani amfuate msanii huyo huko aliko kutokana na mapenzi aliyonayo kwa kazi zake za filamu.

Uamuzi wa binti huyo kujiua haukufanikiwa kwa kuwa aliwahishwa Hospitali ya Tumbi ambako anaendelea na matibabu.

No comments:

Post a Comment