Katika pitapita zangu kwenye blogs mbalimbali leo nimeikuta hii stori inayomhusu msichana maarufu nchini, Elizabeth Michael 'Lulu'
Binti huyo kwa sasa yupo rumande akikabiliwa na kesi mauaji ya msanii maarufu wa filamu nchini, Steven Kanumba.
Ingawa hivi karibuni Lulu alisema hana mpenzi na akaapa kuthibitisha hilo, inadaiwa kuwa alikuwa ni uhusiano wa kimapenzi na Kanumba.
Oktoba mwaka jana alifanya mahojiano na mtangazaji wa Clouds Media Group, Zamaradi Mketema, akayasema hayo hapo chini.........
Msanii Star wa filamu ambae alianza kuigiza akiwa na umri mdogo ameamua kufunguka na kuweka wazi kwamba ana mpango wa kwenda EUROPE kwa sababu moja tu ya kumtafuta JUSTIN BIEBER....
Nilipomuuliza sababu ya kumtafuta kama ni ya kishabiki ama ya kimapenzi alijibu kwamba ni kishabiki lakini lolote pia linaweza kutokea,Lakini hapohapo nikataka kujua kama amesahafanya juhudi zozote za kuwasiliana nae akasema kwasasa bado hapana ila anachotaka kufanya ni hiko kumuendea hukohuko kumsaka..
Kuhusiana na NAULI nilipotaka kujua amejipangaje LULU akasema atachangisha kadi kwasababu anaamini kitendo anachotaka kukifanya ni cha kimaendeleo na ni UJASIRI mkubwa kwasababu amejitosa kwenda kumtafuta mtu ambae hapatikani kirahisi hivyo ni USHUJAA..
Kabla sijamaliza interview nae nilimuuliza lulu ikitokea bahati akakutana nae na mara itokee JUSTIN BIEBER nae amevutiwa na yeye KIMAPENZI, je atakuwa Tayari!!??? alichonijibu ni kwamba YANI BILA KUULIZA YUKO TAYARI KABISA na hilo sio swali la kuuliza kwani bila wasiwasi atafanya hivyo..
Chanzo- Blog ya Zamaradi Mketema
No comments:
Post a Comment