Wednesday, April 18, 2012

Kamati ya mazishi- Kanumba hakuwa tajiri

Kamati iliyoshughulikia mazishi ya aliyekuwa msanii nyota wa filamu nchini Tanzania, Steven Kanumba, imekanusha uvumi kwamba, msanii huyo ameacha mali zenye thamani ya Sh. milioni 700/-.


“Hizi taarifa hazina ukweli ndani yake, ninachojua Kanumba amefariki akiwa na jina kubwa katika sanaa, lakini ni mtu mwenye pesa ya kawaida,” amesema Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Gabriel Mtitu.


Mtitu amesema, kinachozungumzwa na watu hakina ukweli.Mjumbe wa Kamati hiyo, William Mtitu, alisema mali zilizoachwa na marehemu Kanumba ni magari matatu na, viwanja ambavyo hata hivyo, hakutaja idadi yake wala mahali viliko.


Kwa mujibu wa Mtitu, nyumba aliyokuwa akiishi Kanumba, eneo la Sinza, Dar es Salaam alisema kuwa ilikuwa ni ya kupanga.


Alisema, Ksnumba alikuwa akimiliki kampuni inayohusika na uandaaji na utayarishaji wa filamu ijulikanayo kwa jina la “Kanumba The Great” jijini Dar es Salaam.


Mtitu amesema, kampuni hiyo inamiliki studio, inadaiwa kwamba, in mchango mkubwa katika kuinua vipaji vya wasanii chipukizi, akiwamo Wema Sepetu na Elizabeth Michael, maarufu kama ‘Lulu’.


Alikataa kueleza kiasi cha fedha alizoacha Kanumba na akaunti zake za benki kwa maelezo kwamba suala hilo ni la familia.

No comments:

Post a Comment