MWANAFUNZI wa kidato cha tano katika Shule ya Sekondari ya St. Anthony Mbagala, mkoani Dar es Salaam, Franco Donald Kisongo (18), amepotea jijini humo.
Franco ni mgeni jijini Dar es Salaam amepotea tangu Jumapili asubuhi ikiwa ni siku nne tu tangu ajiunge na shule hiyo kuanza masomo ya kidato cha tano.
Kijana huyo aliwaaga wanafunzi wenzake kuwa alikuwa anakwenda kwa shangazi yake Kariakoo, hakufika huko, na pia hakurudi shule na hadi sasa haijulikani alipo.
Shangazi wa kijana huyo, Adelaide Kisongo anaishi katika makutano ya barabara za Uhuru na Sikukuu.
Walimu na walezi wa kijana huyo Mrangi, wametoa taarifa katika vituo vya Polisi Mbagala Kizuiani, Chang’ombe na Msimbazi, na wanatumia RB namba 3343/2012 ya kituo cha Msimbazi kumtafuta.
Kwa yeyote mwenye taarifa kuhusu mahali alipo kijana huyo anaombwa kutoa taarifa kituo chochote cha polisi au kuwasiliana na wenye namba za simu zifuatazo.
0784- 384035, 0717-371763, 0713- 761006, na 0715- 247544
Taarifa zilizopatikana hivi punde ni kuwa, Polisi hawana taarifa za kijana huyo.
No comments:
Post a Comment