Tuesday, March 20, 2012

Mwakyembe- Niacheni, mnawatisha wanangu

Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk Harrison Mwakyembe hataki vyombo vya habari viendelee kuandika taarifa kuhusu afya yake kwa kuwa zinaitisha familia yake.


Mwakyembe amesema ugonjwa unaomsumbua unafahamika kitaalamu kwa jina la Popular Scleroderma, na anasema “Sasa nimepona kabisa.”


Dk Mwakyembe amekuwa akisumbuliwa na maradhi ya ngozi tangu mwaka jana, alikwenda kupata tiba katika Hospitali ya Appolo, India.


“Si kwamba sijambo, bali nimepona kabisa baada ya kugundulika na maradhi hayo na kutibiwa.” amesema jana wakati anazungumza na waandishi wa habari.


“Nimerudi juzi kutoka India na daktari wangu ameniambia nimepona, nilikuwa nasumbuliwa na maradhi ya ‘Popular Scleroderma’ iliyosababisha ‘skin disorder’ (ngozi kutokuwa katika hali ya kawaida), lakini kwa nguvu za Mungu nimepona, namshukuru Mungu.”


“Naomba jamani sasa ugonjwa wa Mwakyembe ufike mwisho kuandikwa. Watu walitarajia na kusubiri mengine, lakini nawaambia mliotaka kuandika vichwa vya habari vya kifo changu mjue tafadhali niko hapa sijafa, naomba yaishe sasa,” alisema Dk. Mwakyembe.

No comments:

Post a Comment