Thursday, March 15, 2012

Hakimu adaiwa kuvunja ndoa za watu kwa barua

Hii ni barua ambayo Joyce Kapushi alipewa aende akapumzike kwa baba yake aitwaye Saidi Kapushi, kwa muda usiojulikana bila ya mumewe kuitwa mahakamani au katika baraza lolote la usuluhishi la kata au mtendaji hata viongozi wa dini ili kujadili lolote kuhusu wanandoa hao.


Hakimu Mfawidhi wa mahakama ya mwanzo Mlowo, wilaya ya Mbozi mkoani Mbeya jina linahifadhiwa anadaiwa kuvunja ndoa za watu kwa kutoa barua za mapumziko kwa wanandoa bila hata kusikiliza mashauri yao mahakamani.


Mwandishi wa habari hii amepata baadhi ya barua ambazo zimekuwa zikiandikwa na makarani wa mahakama hiyo na hakimu huyo kuweka saini yake katika barua hizo.


Hakimu huyo ameufanya mradi endelevu kwa wanawake ambao humpatia fedha kupitia makarani wake.


Inadaiwa kwamba, wanawake wamekuwa wakishinikiza wapewe barua za kwenda mapumziko kwa wazazi wao kwa muda usiojulikana.


Hivi karibuni, Joyce Kapushi alipewa barua ya kwenda kupumzika kwa baba yake aitwaye Saidi Kapushi, kwa muda usiojulikana.


Inadaiwa kuwa, zaidi ya barua saba zimeandikwa na hakimu huyo kwa kipindi cha miezi mitatu, na kwamba, wanaume wamekuwa wakiishi katika mateso kutokana na manyanyaso ya wanawake hao wakishirikiana na hakimu huyo anayependa kutembelea gari jekundu aina ya Suzuki.


Chanzo: Blog ya Mbeya Yetu

No comments:

Post a Comment