Monday, February 20, 2012

Akutwa amekufa chumbani kwake Mbeya

Mtu aliyefahamika kwa jina la Rashid Mtila (35), mkazi wa Kata ya Manga jijini Mbeya amekutwa amekufa chumbani kwake.



Mwili wa marehemu umegunduliwa na watu wawili waliokuwa wakienda kunywa pombe za kienyeji katika moja ya nyumba iliyopo katika eneo hilo maarufu kama Jua Kali Mwanjelwa, majira ya saa sita mchana Februari 19.




Kwa mujibu wa Balozi wa mtaa huo, Godwini Kitwika, alitoa taarifa kwa Diwani wa kata hiyo ya Manga, Daniel Mwakisyala naye alitoa taarifa katika kituo cha polisi cha Mwanjelwa.



Mtila alikuwa akiishi peke yake, hivi karibuni katika kituo cha mabasi cha Mwanjelwa kwa kile kilichodhaniwa kuwa ni ugonjwa wa kifafa, na siku mbili zilizopita alianguka mara tatu hali iliyomlazimu kwenda kupumzika chumbani kwake.



Baada ya kifo hicho, vijana wa mtaa huo walipitisha mchango wa dharura kwa ajili yakupata shuka ili kumuhifadhia marehemu huyo.




Kwa mujibu wa Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya, Advocate Nyombi, ameruhusu mwili wa marehemu kuchukuliwa na ndugu zake kwa ajili ya mazishi.




Chanzo: Bombafm.blogspot.com

No comments:

Post a Comment