Thursday, January 26, 2012

Mume adaiwa kumpiga mkewe, kumwingiza chupa sehemu za siri

Bi Judith Mnyape (32) mkazi wa Ghana Magharibi jijini Mbeya anadaiwa kupigwa na mumewe, Clemence Luhimbo (36), maarufu kwa jina la Kidevu na kujeruhiwa sehemu mbalimbali za mwili wake kwa kile kilichodaiwa na kuwa ni wivu wa kimapenzi.


Tukio hilo limetokea Januari 14, mwaka huu saa 2 usiku nyumbani kwake wanapoishi.


Inadaiwa kuwa, dereva huyo wa teksi alimpiga mkewe kwa kutumia ufagio hadi kuvunjika hicyo kusababisha mwanamke huyo apate majeraha na kulazwa katika hospitali ya Rufaa jijini Mbeya Januari 20 hadi 21 mwaka huu.


Inadaiwa kuwa, licha ya kumpiga mkewe, Luhimbo, alimfungia mkewe kwa muda wa siku tatu mfululizo bila kumpa huduma yoyote ya matibabu.


Kuna madai kwamba, mbali na kumfungia, Luhimbo pia alimwingiza chupa ya soda kwa siku tatu mfululizo mkewe sehemu za siri kwa madai kuwa amechoshwa na vitendo vya ukahaba vinavyofanywa na mkewe.


Luhimbo anahojiwa na Kituo cha Polisi cha Kati, kitengo cha kupinga ukatili dhidi ya wanawake na watoto, mpaka sasa wamemtaka kuhakikisha mkewe anapatiwa matibabu ipasavyo, huku akiendelea kuripoti polisi.


Habari kwa hisani ya blog ya Mbeya yetu

No comments:

Post a Comment