Rahabu Robert (26) mkazi wa mtaa wa Manga A, jijini Mbeya amekutwa amemfunga kamba ya katani kwenye meza mtoto wake wa kumzaa aitwaye Eliza Frank (4), kwa kile alichodai kuchoshwa na tabia mbaya ya uzurulaji.
Tukio hilo limetokea Januari 25, mwaka huu nyumbani hapo saa 10 jioni na mtoto huyo kukutwa majira ya saa 12 jioni na majirani wakati mama huyo akiwa kanisani kwenye ibada.
Baada ya majirani kubaini ukatili huo walimtaarifu Mwenyekiti wa mtaa Bi Rose Mwaisanga, alimfuata mama huyo kanisani katika Kanisa la Moravian Ruanda lililopo karibu na Hospitali ya K'S lililopo mtaa wa Mafiati.
Baada ya kufika nyumbani mama huyo na mwenyekiti walimkuta mtoto huyo akilia kwa uchungu kutokana na maumivu makali ya kamba hiyo.
Walimfungua kamba mtoto huyo, mama yake akapelekwa katika kituo cha Polisi cha Kati.
Mwenyekiti wa mtaa huo Bi Rose na mwandishi wa habari hizi walikuwa na wakati mgumu wa kumnusuru mama huyu asipigwe na wananchi wenye hasira kali.
Wananchi hao walikuwa wakimpiga mama huyo bila kujali mtoto mchanga aliyembeba mgongoni.
aliingizwa kwenye daladala hali ambayo ilisababisha wananchi hao kuipiga mawe daladala hiyo wakidai mama huyo naye aadhibiwe.
Baba mzazi wa mtoto huyo Bwana Frank Anangisye (29), amesema, alikuwa hana taarifa yoyote juu ya mateso ya mwanae na kuwashukuru majirani kwa kuweza kufichua uovu wa mkewe.
Mama wa mtoto huyo Bi Rahabu anatarajiwa kufikishwa mahakamani wakati wowote baada ya uchunguzi wa Jeshi la polisi kukamilika.
Habari kwa hisani ya blog ya Bombafm
No comments:
Post a Comment