Tuesday, August 9, 2011

Makamba- Pinda toa tamko kuhusu mafuta


January Makamba


Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini imemtaka Waziri Mkuu, Mizengo Pinda atoe tamko kuhusu mgomo wa wafanyabiashara ya mafuta.


Mwenyekiti wa kamati hiyo, January Makamba ameishangaa Serikali kwa kuwa kimya kwa kuwa tatizo hilo lipo kwa takribani wiki moja sasa.


"PM (Waziri Mkuu) sema kitu" amesema Januari wakati akiliomba Bunge lijadili tatizo la upatikanaji mafuta kama jambo la dharura.


Hali ya upatikanaji wa mafuta nchini ni mbaya, na kwa mujibu wa Makamba, katika baadhi ya maeneo lita moja inauzwa Sh. 3,000/-, 4,000/- na 5,000/-


Mbunge huyo amesema, bei ya mafuta lazima ishuke kati ya leo hadi kesho asubuhi.


Amesema, Serikali inapaswa kuonesha kuwa ipo na ina uwezo wa kusimamia sheria.


Amesema, Serikali inapaswa kutoa tamko kwa kuwa mafuta ni muhimu kwa uchumi na usalama wa nchi.


“Nataka Serikali ijaribu kuonesha kuwa ipo… tunaposema nchi itasimama ni kweli itasimama ” amesema Makamba na kuhoji kwamba, tangu mwaka 2,000 Serikali imekuwa ikipanga bei za mafuta, kwa nini limekuwa tatizo sasa?

No comments:

Post a Comment