Monday, July 25, 2011

USALITI

Jamaa ana mpenzi, wakiwa pamoja na wanavyoelezana ni kuwa wanapendana kiukweli kiasi kwamba hata passwords za bank cards,na za e-mail wamepeana.


Wameahidiana kuwa hawatasalitiana milele kamwe!


Wapenzi hawa wana ujuzi wa kutumia mitandao ya kijamii, siku moja wakajikuta wanachati kwenye thread wakitumia majina ya bandia.


Na kila mmoja hakujua anachat na nani na ikafika point wakakubaliana wawe wapenzi kwa sababu, kila mmoja alimwambia mwenzake kuwa alikuwa single.


Mambo yakaendelea, wakirudi home kila mtu akijifanya mtakatifu, wakaoneshana mapenzi motomoto.


Wakiachana kwenda kazini kila mmoja akawa anachat na 'mpenzi mpya' na wakakubaliana kwamba umefika muda wakutane na 'kufahamiana zaidi'.


Mwanaume akampa location mwanamke kwamba akae sehemu tax itakuja kumchukua na kumpeleka hotelini, na atamwambia yupo chumba gani.


Siku ya 'uzinduzi' a.k.a kukata utepe ikawadia, mdada akaenda alipoelezwa, tax ikaenda kumchukua kumpeleka kwa 'mpenzi mpya'.


Gari likafika hotelini, dada akapelekwa kaonyeshwa chumba,kagonga mlango, ukafunguliwa................guess what happened!!!!!


Niambie nini kiliendelea hapo, kama ni kesi itapelekwa mahakama gani?

No comments:

Post a Comment