Thursday, June 23, 2011

Pinda kaacha kutumia Mercedes Benz

Waziri Mkuu wa Tanzania, Mizengo Pinda ameacha kutumia magari yenye gharama kubwa.


Wananchi na baadhi ya wabunge wamekuwa wakilalamika kuwa viongozi wa juu wa Serikali, wanatumia magari ya kifahari hivyo kuongeza gharama za kuendesha Serikali.


Waziri Mkuu, ameacha kutumia magari aina ya Mercedes Benz na Toyota Land Cruiser VX na sasa anatumia Toyota Land Cruiser GX.


Gharama za kununua na kuyahudumia magari ya Benz na VX ni kubwa sana kulinganisha na gharama za GX.

No comments:

Post a Comment