MWANAUME nchini Uingereza amepandishwa kizimbani akidaiwa kumuua mpenzi wake aliyemkebehi kuwa ana uume mdogo sana hivyo hawezi kumtosheleza hamu yake ya ngono.
Peter Ling, 50, ameieleza mahakama kuwa alishindwa kuzitawala hasira zake baada ya kipenzi chake Linda Casey kumuambia kuwa hana uume mkubwa wa kuweza kumtosheleza hamu yake wakati wa kujamiiana, limeripoti gazeti la Daily Mail la Uingereza.
Ling, aliandaa sehemu ya starehe jijini London kwa ajili ya kukutana na Linda akiwa na nia ya kumuuliza kama Linda ana mwanaume mwingine a.ka. king'ast.
Walikutana, wakavunja amri wa ya sita, ndipo Ling alipomgeukia Linda na kuanza kumhoji kuhusiana na emails alizozituma zinazohusiana na tovuti za kutafuta wachumba na pia kama ana king'ast.
Kulikuwa na mabishano, Linda aliongelea masuala ya viungo vya siri vya Ling akimueleza kwamba uume wake ni mdogo sana kuweza kumtosheleza.
"Nilikuwa ni kama bomu lililokuwa likisubiria kulipuka wakati wowote, alipotoa maoni hayo moja kwa moja yalizama kwenye akili zangu", Ling aliieleza mahakama.
"Siku zote nimekuwa nikiushuku ukubwa wa uume wangu", aliongeza Ling.
Baada ya Linda kusema hivyo Ling alianza kumshushia kipigo Linda hadi mwanamke huyo akaaga dunia.
Ling ameiomba mahakama iamue kesi hiyo kuwa ni ya mauaji bila kukusudia na si kesi ya mauaji ya kukusudia.
No comments:
Post a Comment