Monday, February 22, 2010

Mtoto asiyependa kula

MDAU aliomba ushauri kwa mtoto asiependa kula, kapata 'msaada kwenye tuta', si vibaya nawe ukiipata elimu hii.
Matatizo ya mtoto kutopenda kula ni mengi yanaweza kusababishwa na tabia binafsi au maradhi.
Kama mtoto yuko salama hana maradhiila hapendi tu kula kazi ni ndogo sana kumbadilisha ili apende kula.

Inawezekana unandaa chakula kizuri lakini bado mtoto anasumbua kula ili kumbadilisha tabia apende kula.
Unatakiwa kumtengenezea kwanza hamu ya kula maana bila ya kuwa na hamu ya kula hata chakula kiwe kizuri vipi huwezi kula vizuri.

Hamu ya kula iandaliwe kuanzia asubuhi unapofungua kinywa, tengeneza chai ya rangi au ya maziwa, weka tangawizi ya unga kwenye nusu lita ya maji au maziwa.
Weka tangawizi kijiko kidogo cha chai mzoweshe mwanao chai hii kila siku asubuhi,tangawizi ni kiungo kizuri kinachosaidia kumengenya chakula tumboni na kusababisha njaa haraka na hamu ya kula.

Hapo utakua umemtengenezea mtoto hamu ya kula mchana.
Ili kumuandalia mtoto hamu ya kula chakula cha usiku tengeneza juisi ya Pasheni au Embe au Nanasi au tunda lolote, kumbuka kuchanganya tena kijiko kidogo cha chai kilichojaa tangawizi na usage pamoja na mchanyanyiko wako.
Mpe mtoto glasi moja ya Juice kabla ya kula, utaona mabadiliko, usimpatie baada ya kula maana itamsababishia njaa.

Ukifuata maelekezo vizuri utaona mabadiliko ndani ya siku moja tu.

1 comment:

  1. Asante sana kwa ushauri wako. kwani hata mie mtoto wangu hapendi kula.je na kwenye uji pia tuweke hiyo tangawizi? kwani hata ujin hapendikunywa.

    ReplyDelete