Friday, July 17, 2009

Tevez analitaka jumba la Ronaldo





Christiano Ronaldo(24) anauza jumba lake la kifahari lililopo kwenye eneo la vibopa, Cheshire nchini Uingereza.
Nyota huyo wa soka duniani anataka Paundi milioni tano ili aliachie jumba hilo lenye kila kitu unachoweza kukihitaji kwenye nyumba vikiwamo vyumba vitano vya kulala, bwawa la kuogelea, sauna na jakuzi.
Ronaldo alilinua paundi milioni nne miezi 18 iliyopita, aliyekuwa mchezaji mwenza Man United, Carlos Tevez kaonesha nia ya kulinunua.
Tevez ameshakwenda kuliona, huenda ataenda kuishi hapo wakati huu anapoanza maisha mapya akiwa na Man City.
Ronaldo anakwenda kuishi Madrid, Hispania, Man U imemuuza kwa Paundi za Uingereza milioni 80 ambazo ni sawa na zaidi ya sh BILIONI 160 za Tanzania.

No comments:

Post a Comment